Searching...
Tuesday, January 25, 2011

Maharamia wa Somalia wateka nyara meli ya Ujerumani


Maharamia wa Somalia wameteka nyara meli ya MV Beluga Nominations mali ya Ujerumani ikiwa na mabaharia wa nchi mbalimbali kwenye maji ya visiwa vya Ushelisheli.
Meli hiyo ilitekwa nyara jana Jumatatu kwenye umbali wa kilomita 100 nje ya visiwa vya Ushelisheli ikiwa na mabaharia 12 wakiwemo raia wa Ukraine, Ufilipino, Wapoland na Warusi.
Taarifa hiyo imetolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Ukraine ambayo hata hivyo haikutoa idadi hasa ya raia wa kila nchi.
Karibu mabaharia 1,200 walitekwa nyara na maharamia wa Somalia mwaka 2010 idadi ambayo Ofisi ya Kimataifa ya Vyombo vya Baharini imesema ni ya kutisha.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!