Searching...
Wednesday, January 12, 2011

Mafuriko ya Australia; maelfu wayahama makaazi yao

 Maelfu ya watu wameanza kuondoka katika vitongoji vya mji wa Brisbane, ambao ni wa tatu kwa ukubwa nchini Australia, huku wengine wakikusanya magunia yenye mchanga mbele ya nje ya nyumba zao ili kuzuia maji na kuhifadhi chakula kufuatia kushadidi kwa mafuriko na mvua kubwa nchini humo. Watu wengi wameihama mitaa ya Brisbane katika jimbo la Queensland, huku vitongoji 80 vikitazamiwa kukumbwa na mafuriko, iwapo kingo za mto Brisbane zitaachana kama inavyotazamiwa hapo kesho. Nyumba zipatazo elfu 20 zinatazamiwa kuathiriwa na mafuriko katika siku chache zijazo. Hayo yamesemwa leo na Anna Bligh , gavana wa jimbo la Queensland.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!