Searching...
Thursday, December 9, 2010

Msafara wa Asia wa misaada ya kibinadamu kwa ajili ya Gaza wawasili Iran

 Msafara wa misaada ya kibinadamu ya watu wa Asia kwa ajili ya raia wanaozingirwa na utawala haramu wa Israel wa Ukanda wa Gaza umewasili nchini Iran ukiwa njiani kuelekea Palestina. Msafara huo ulioanzia India umeingia katika ardhi ya Iran kupitia mpaka wa nchi kavu wa Pakistan na utapita katika nchi za Uturuki na Syria kabla ya kuelekea Misri na kuingia Gaza kupitia kivuko cha Rafah. Msafara huo unaobeba misaada ya kitiba na dawa unayashirikisha mashirika 125 ya misaada ya kibinadamu kutoka nchi za India, Pakistan, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Indonesia, Malaysia, Uturuki na nchi nyingine kadhaa za Asia. Wanaharakati wa kutetea haki za binadamu na waandishi habari pia wanashiriki katika msafara huo unaokusudia kuvunja mzingiro wa pande zote wa utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya raia milioni moja na nusu wa Ukanda wa Gaza huko Palestina.v

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!