Searching...
Monday, December 6, 2010

Marais wa Misri na Tanzania wasisitiza juu ya kuimarishwa usalama Afrika

 Marais wa Tanzania na Misri wamesisitiza juu ya udharura wa kuchukuliwa hatua za kuongezwa ustawi barani Afrika sambamba na kuimarisha amani na uthabiti wa bara hilo. Marais Hosni Mubarak na Jakaya Mrisho Kikwete wa Tanzania wamesema hayo katika mazungumzo yao mjini Cairo Misri na kusisitiza azma ya nchi zao ya kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi. Aidha ajenda kuu ya mazungumzo ya viongozi hao ilikuwa ni suala la matumizi ya maji ya Mto Nile ambalo limezua mjadala mkubwa. Misri inatofautiana na nchi nyingine za kando kando ya Mto Nile kuhusiana na matumizi ya maji ya mto huo. Miezi kadhaa iliyopita nchi za Tanzania, Kenya, Ethiopia, Uganda na Rwanda zilitia saini makubaliano yanayosisitiza juu ya kugawana maji ya Mto Nile kwa uadilifu zaidi. Nchi hizo zinatarajia kuwa makubaliano hayo mapya yatachukua nafasi ya mkataba wa zamani uliotiwa saini katika kipindi cha ukoloni. Makubaliano hayo ya zama za ukoloni yanazipa Misri na Sudan asilimia karibu 80 ya maji ya Mto Nile. Misri na Sudan zimekuwa zikipinga makubaliano mapya ya maji ya mto huo.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!