Searching...
Tuesday, November 30, 2010

Wasiwasi wazuka Kenya baada ya Waziri Mkuu kuamuru wasenge wakamatwe

Wasiwasi umezuka nchini Kenya baada ya Raila Odinga Waziri Mkuu wa nchi hiyo kutoa amri ya kukamatwa wasenge na wasagaji. Nguru Karugu mjumbe wa jumuiya ya watu wanaojamiiana wakiwa wa jinsi moja ya Kenya amesema leo kuwa, jamii ya watu hao nchini Kenya imekubwa na kiwewe na wasiwasi mkubwa baada ya kutolewa amri ya kuwakamata.
Odinga alisema hapo jana kuwa, vitendo vya wasenge na wasagaji si vya kawaida, na kwamba ni wendawazimu kwa mwanamume kutaka kufanya ngono na mwanamume mwenzake kwani sensa ya hivi karibuni inaonyesha kwamba wanawake ni wengi zaidi kuliko wanaume nchini Kenya. Waziri Mkuu wa Kenya pia aliongeza kwamba hakuna haja ya wanawake kujiingiza katika usagaji kwani jukumu lao katika jamii ni kuzaa watoto. Aidha aliukosoa mrengo wa 'Hapana' uliopinga Katiba mpya kwa kuwapotosha wananchi wakati wa kampeni kwa kusema kuwa Katiba mpya inaunga mkono vitendo vya kujamiiana watu wa jinsia moja.
Amri ya kukamatwa watu wanaotenda vitendo hivyo vichafu imetolewa miezi michache baada ya Waziri wa Mipango Maalumu wa Kenya Ester Murufi kuamsha hasira za Wakenya pale alipotoa wito wa kutambuliwa rasmi na kukubaliwa wasenge na wasagaji nchini humo.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!