Searching...
Friday, November 19, 2010

Shule zilizojengwa kwa msaada wa China zaboresha miundo mbinu ya elimu nchini Kenya

Waziri wa elimu wa Kenya Bw. Sam Ongeri tarehe 17 kwenye sherehe ya kuzikabidhi shule za msingi za vijijini kwa Kenya alisema, shule hizo zilizojengwa kwa msaada wa China zinaboresha miundo mbinu ya elimu nchini Kenya.
Bw. Ongeri alisema ujenzi wa miundo mbinu ya elimu nchini Kenya bado uko nyuma, na shule za hivi sasa haziwezi kukidhi mahitaji ya ongezeko la idadi ya wanafunzi. Shule hizo mbili zilizojengwa kwa msaada wa China zote ziko katika sehemu zenye idadi kubwa ya watu, hii itatoa urahisi kwa watoto wa huko kwenda shule.
Balozi wa China nchini Kenya Bw. Liu Guangyuan alieleza matumaini kuwa watu wa huko watanufaika na shule hizo mbili, na wakenya wengi zaidi watanufaika na ushirikiano wa kirafiki wa muda mrefu kati ya China na Afrika.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!