Searching...
Thursday, November 25, 2010

China yashikilia kuongeza uwezo wa kujiendeleza wa Afrika



Mjumbe maalumu wa serikali ya China anayeshughulikia mambo ya Afrika Bw. Liu Guijin alisema China inapenda kujikita katika kuongeza uwezo wa kujiendeleza wa nchi za Afrika, na kuzisaidia kutimiza malengo ya maendeleo ya milenia.
Huu ni mwaka wa maadhimisho ya miaka 10 tangu baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika lianzishwe na pia ni maadhimisho ya miaka 40 tangu China na Ethiopia zianzishe uhusiano wa kibalozi, ubalozi wa China nchini Ethiopia na idara ya utafiti wa amani na maendeleo ya kimataifa nchini Ethiopia hivi karibuni huko Addis Ababa walifanya mkutano wa kujadili uhusiano wa kunufaishana kati ya China na Ethiopia na China na Afrika.
Kwenye mkutano huo, Bw. Liu alisema China inaendeleza uhusiano kati yake na Afrika chini ya kanuni na msingi wa usawa, kunufaishana na kupata maendeleo kwa pamoja. China inapenda kupanua ushirikiano wake na Afrika katika mambo ya biashara, uwekezaji na kilimo kutokana na uzoefu wake wa kujiendeleza.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!