Searching...
Monday, November 15, 2010

Burundi yaiunga mkono Misri kuhusu matumizi ya maji ya mto Nile

 Muhammad Rukara mshauri maalum wa Rais wa Burundi leo amesema, serikali ya Bujumbura haitachukua msimamo dhidi ya Misri kuhusu makubaliano mapya ya nchi zilizoko pembezoni mwa mto Nile, ambayo yatatiwa saini na baadhi ya nchi.
Rukara ameongeza kuwa, Burundi siku zote itakuwa pamoja na Misri. Mshauri huyo wa rais wa Burundi vilevile amesema baada ya kukutana na Rais Husni Mubaraka wa Misri kwamba, wana matumaini nchi zote zilizoko pambizoni mwa Mto Nile zitachukua maamuzi ya pamoja yatakayodhamini maslahi ya wote katika mazungumzo ya jumla yatakayofanyika hivi karibuni. Nchi zilizoko pambazoni mwa Mto Nile ni Uganda, Ethiopia, Sudan, Tanzania, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Burundi, Rwanda, Kenya na Misri.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!