Searching...
Saturday, November 6, 2010

61 wauawa katika mlipuko wa bomu katika msikiti mmoja nchini Pakistan

 Kwa  hakika watu 61 wamepoteza maisha yao na wengine takribani mia moja kujeruhiwa baada ya kutokea mlipuko katika msikiti mmoja kaskazini magharibi mwa Pakistan. Mlipuko huo wa bomu umetokea wakati wa waumini walipokuwa wakitekeleza ibada ya Sala ya Ijumaa katika eneo la Darra Adam Khel jirani na eneo moja la kikabila nchini humo.
Taarifa zaidi zinasema kuwa, hali ya baadhi ya majeruhi ni mbaya na kuna uwezekano wa kuongeza idadi ya vifo. Kundi la wanamgambo wa Taliban limetangaza kuhusika na shambulio hilo la kigaidi. Msikiti huo unapatikana katika kijiji cha Akhurwal yapata kilomita 45 hivi kusini mwa Peshawar.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!