Searching...
Wednesday, October 13, 2010

WHO inahofia idadi ya watoto wanaoathirika na vita Somalia

Shirika la afya duniani WHOlimeelezea hofu yake kuhusu ongezeko la idadi ya watoto wanaojeruhiwa katika vita mjini Moghadishu Somalia.
Watoto nchini Somalia
Watoto nchini Somalia
WHO inasema zaidi ya watoto 1000 wamejeruhiwa mjini Moghadishu tangu mwezi Januari mwaka huu. Vita vya miongo miwili nchini humo vimesambaratisha kabisa huduma za afya na kulifanya shirika la WHO kuanzisha mradi wa kufufua baadhi ya vituo vya afya ili kuvisaidia kukabiliana na idadi kubwa ya majeruhi ambao ni watoto. Paul Garwood ni msemaji wa WHO mjini Geneva.

Kwa mujibu wa makadirio ya WHO Somalia ina madaktari waliofuzu wapatao 250. Na vituo vya afya nchini humo kila wakati vinakabiliwa na upungufu mkubwa wa madawa, vifaa vya matibabu na wataalamu wa afya.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!