Searching...
Saturday, October 23, 2010

Waganda 20 wamekufa kutokana na ugonjwa wa tekenya miezi 2 iliyopita

 Wizara ya Afya nchini Uganda imesema kuwa takriban raia wake 20 wamefariki dunia katika kipindi cha miezi 2 iliyopita kutokana na ugonjwa wa tekenya. James Kakooza, Waziri wa Huduma za Afya wa nchi hiyo amesema, wengi wa waliokufa kutokana na ugonjwa huo unaotokana na funza mfano wa kiroboto ni watoto wadogo. Kakooza amesisitiza umuhimu wa kutopuuzwa vita dhidi ya funza na kusema kuwa, Waganda wengine zaidi ya 20,000 tayari wameathiriwa na ugonjwa huo. Ameongeza kuwa, watu wengi wamekuwa wakipuuza umuhimu wa kutafuta matibabu wanapoingiwa na kidudu hicho ambacho husababisha vifo vya mapema kwa watu wazima ambao wanaugua magonjwa mengine. Funza huyo humuingia mwanadamu mara nyingi kupitia nyayoni, kumfyonza damu na kisha kusababisha baadhi ya viungo vyake kuoza.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!