
Mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Congo amekaribisha kutiwa nguvuni kwa kiongozi wa kundi la Mai Mai Cheka akisema kuwa ni ushindi wa haki na uadilifu. Margot Wallstrom ambaye ni mtaalamu wa masuala ya ubakaji anayetembelea Congo amesema kutiwa nguvuni Kanali Mayele ni ushindi mkubwa wa uadilifu hususan kwa wanawake waliobakwa na kunajisiwa. Amesema kuwa kutiwa nguvuni mhalifu huyo ni ishara kwamba wahalifu wengine hawataweza kukimbia mkono wa uadilifu.
Kiongozi wa kundi la Mai Mai Cheka Luteni Kanali Mayele anatuhumia kwamba aliongoza kundi la watu mia mbili na wapiganaji wa Kihutu kutoka Rwanda katika mashambulizi yaliyolenga vijiji 13 vya eneo la Walikale katika jimbo la Kivu Kusini ambapo wanawake 500, watoto wadogo na hata wanaume walibakwa na kunajisiwa. Hujuma hiyo ilifanyika katika kipindi cha mwishoni mwa mwezi Julai hadi mwanzoni mwa Agosti.
0 comments:
Post a Comment