Searching...
Saturday, October 16, 2010

UN: Bado watu bilioni 1 ulimwenguni wanakabiliwa na baa la njaa

 Ulimwengu leo hii unaadhimisha Siku ya Chakula Duniani, katika hali ambayo Umoja wa Mataifa umesema bado zaidi ya watu bilioni 1 kote duniani wanasumbuliwa na baa la njaa. Katika ujumbe wake wa leo, Ban Ki-Moon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametoa wito kwa mifumo ya uzalishaji wa chakula duniani kuzidisha kasi ya kuuhakikishia ulimwengu usalama wa chakula. Ban Ki-Moon amesema, dunia yenye njaa, haiweza kuvunja minyororo ya uchochole na itapatwa kwa wepesi na magonjwa mbalimbali. Katibu wa UN ameashiria udharura wa watoto kupewa kipaumbele katika suala hilo ili wakulie katika mazingira mazuri ya kupata elimu bora itakayowafaidi katika siku za usoni.
Takwimu zilizotolewa hivi karibuni na Shirika la Global Hunger Index zinaonyesha kuwa, mataifa 25 hususan za barani Afrika kati ya mataifa 122 yaliyohusishwa kwenye uchunguzi huo kote duniani yanasumbuliwa na baa la njaa.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!