Searching...
Friday, October 22, 2010

Mkutano wa baraza la haki za binadamu wajadili kuhusu suala la haki za binadamu

Mkutano wa tatu wa baraza la haki za binadamu la Beijing umefanyika tarehe 20 Oktoba mjini Beijing, na masuala yanayozungumzwa zaidi ni jinsi ya kushughulikia matatizo yanayoikabili dunia nzima na namna ya kulinda haki za binadamu.  
Naibu mkuu wa Chuo Kikuu Hei Longjiang cha China Bi. He Ying anaona kuwa jumuiya ya kimataifa inapaswa kufanya mazungumzo, mawasiliano na ushirikiano kwa kufuata sheria za haki za binadamu za kimataifa, ili kuhakikisha haki za binadamu zinaheshimiwa na kulindwa vizuri zaidi.
Mtaalamu wa Taasisi ya sayansi ya jamii ya China Bw. Huo Guihuan amesema, kila nchi ina hali yake, na kiwango cha maendeleo na mawazo kuhusu haki za binadamu pia kinatofautiana.
Naibu mkuu wa Taasisi ya utafiti wa haki za binadamu ya China Bw. Dong Yunhu anaona kuwa, hali ya haki za binadamu imepata mabadiliko makubwa nchini China tokea sera ya mageuzi na ufunguaji mlango ianze kutekelezwa, na hivi sasa hali ya haki za binadamu ya China iko katika kipindi kizuri zaidi katika historia yake nchini China.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!