Searching...
Thursday, October 28, 2010

Maafa ya tsunami, tetemeko la ardhi na mlipuko wa volkano ya Indonesia

Mpaka sasa maafa ya tsunami na tetemeko la ardhi yaliyotokea nchini Indonesia yamesababisha vifo vya watu 272, na wengine zaidi ya 400 hawajulikani walipo; na idadi ya vifo vilivyosababishwa na mlipuko wa volkano nchini humo pia imefikia 30. maafa hayo kwa ujumla yamesababisha vifo vya watu zaidi ya 300.
Ofisa wa kituo cha usimamizi wa maafa cha Sumatra ya magharibi cha Indonesia Bw. Ade Edward tarehe 27 alisema, hivi sasa kazi za uokoaji zinaendelea katika visiwa vya Mentawai, ambapo miili 272 imegunduliwa, na kuna watu wengine 412 bado hawajulikani walipo. Aidha, wakazi elfu 42 wa sehemu zilizoko karibu na volkano Gunung Merapi iliyoko katikati ya kisiwa cha Jawa wamehamishwa kwenye makazi ya muda yaliyo karibu na mji Yogyakarta. Hata hivyo bado kuna baadhi ya wakazi wanaokataa kuhama kwenye sehemu hiyo.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!