Searching...
Wednesday, September 22, 2010

Waziri mkuu wa serikali ya mpito ya Somalia ajiuzulu

Waziri mkuu wa serikali ya mpito ya Somalia Bw. Umar Abdirashid Sharmarke tarehe 21 alitangaza kujiuzulu, ili kuzuia hali ya kukwama ya kisiasa kuzidi kuwa mbaya nchini Somalia.
Rais Sheikh Sharif Ahmed wa nchi hiyo alipokea uamuzi huo wa Bw. Sharmarke, na kumshukuru kwa kuchukua uamuzi huo wa kulinda serikali ya mpito.
Mwezi Mei mwaka huu, rais Ahmed alitangaza kumteua waziri mkuu mpya, lakini Bw. Sharmark alipinga uteuzi huo, akisema unakiuka katiba ya nchi hiyo.
Habari nyingine zinasema ofisa wa serikali ya mpito ya Somlia tarehe 20 alithibitisha kuwa, mtu mmoja wa kundi la upinzani siku hiyo asubuhi alifanya shambulizi la mabomu la kujitoa mhanga dhidi ya Ikulu mjini Mogadishu, na kusababisha kifo chake na kumjeruhi askari mmoja .

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!