Anasema kila mwaka maelfu ya watu hasa wanawake na watoto wananyanyaswa na wahalifu wanaowatumia kwajili ya kufanya kazi kwa nguvu au biashara ya ngono. Anasema kila nchi inahusika kwa njia moja au nyingine ikiwa ni mahala watu wanakochukuliwa, au kituo cha kupita au nchi wanakopelekwa kuuzwa watu.Bw Ban anasema hatua muhimu zimefanyika tangu Jumuia ya Kimataifa kuanza kupambana na janga hili miaka kumi iliyopita, lakini anasema kuna kazi zaidi zinahitajika.
"Njia pekee ya kukomesha biashara haramu ya binadamu ni kwa kufanya kazi pamoja, kwa ushirikiano kati ya mataifa na jumuia za kikanda, ushirikiano ndani ya Umoja wa Matiafa chini ya kundi la kuratibu ushirikiano wa idara mbali mbali, katika kupambana na biasharab haramu ya watu".
Katibu Mkuu anasema Mpango wa kuchukuliwa hatua utaasaidia kuzuia biashara ya watu, kuwahukumu wahalifu wa biashara hiyo na kuwalinda waathiriwa.


0 comments:
Post a Comment