Searching...
Friday, August 20, 2010

Vita vya Irak vyamalizika rasmi

 

Miaka saba baada ya kumwangusha Saddam Hussein, Marekani imeviondoa vikosi vyake vya mapambano kutoka  Irak na vilivyobakia  vilivuka mpaka alfajiri ya leo na kuingia Kuwait.Ulikuwa usiku wa kihistoria.  Kwa usemi mwingine vita vimemalizika nchini Irak.
Rais Barack Obama ameitekeleza ahadi yake.Alitamka wazi kwamba hadi tarehe 31 mwezi agosti mwaka 2010 jukumu la mapambano kwa majeshi ya Marekani litamalizika nchini Irak. Alisema na hilo ndilo hasa tutakalolifanya,kwa saa iliyopangwa juu ya alama, kama jinsi ilivyoahidiwa.
Saa mbili za usiku jana vyombo vya habari vya  Marekani vilitangaza kwa wakati mmoja mwisho  wa mapambano kwa vikosi vya Marekani katika vita vya Irak.
Muda mfupi tu baadae wizara ya mambo ya nje  ya Marekani ilitangaza rasmi mwisho wa vita kwa majeshi ya Marekani nchini Irak.
Taarifa iliyotolewa na wizara hiyo imezungumzia juu ya wasaa wa kihistoria.
Ilikuwa furaha kubwa kwa askari wa mwisho alfu 2 wa Marekani wakati walipouvuka mpaka na kuingia Kuwait. Askari hao waliruka kutoka  kwenye vifaru na kuanza kupepea bendera  ya Marekani.
Zoezi la kuviondoa vikosi vya mapambano kutoka Irak limekuja mapema kuliko iliyvotarajiwa.Hadi tarahe mosi ya mwezi wa agosti mapambano yalipangwa kumalizika.
Kwa kuyaondoa majeshi hayo,rais Obama ameitekeleza ahadi aliyoitoa juu ya sera za nje, yaani kuvimaliza vita vya Irak kwa njia  ya busara. Obama alivipinga vita vya Irak kabla hata ya kuingia katika madaraka ya urais.
Hatua ya kuyaondoa majeshi mapema imekuja wakati mzuri kwa rais Barack Obama, yaani  kabla ya kufanyika uchaguzi wa bunge.Obama alisema,kuwa hadi mwishoni mwa mwezi huu wanajeshi wa Marekani 9,000 watakuwa wameondolewa kutoka Irak.
Lakini wachunguzi wametilia maanani kwamba  askari hao wanaondoka wakati ambapo raia wengi wa Irak wanauawa.Mwezi uliopita  ulikuwa mbaya sana nchini Irak. Raia 535  waliuawa. Idadi hiyo haijawahi kufikiwa katika  kipindi cha miaka miwili iliyopita.Na jana tu watu zaidi ya 50 waliangamizwa katika mji wa  Baghdad baada ya mshambuliaji wa kujitoa mhanga kujiripua.
Majeshi ya Marekani pia yanaondoka wakati ambapo wairaki bado hawajafanikiwa kuunda serikali, miezi mitano baada ya kufanyika uchaguzi mkuu.Lakini rais Obama amesema kuwa askari wa mwisho kabisa ataondoka Irak  tarehe mosi desemba mwaka ujao-2011.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!