Searching...
Friday, August 27, 2010

Dawa bandia zakamatwa Afrika

Interpol yakamata madawa bandia katika bara la Afrika.
Interpol yakamata madawa bandia katika bara la Afrika.
Polisi wa kimataifa-Interpoli wanasema tani 10 za madawa bandia na wasambazaji wake wamekamatwa na polisi huko Afrika na zaidi ya watu 80 wako chini ya ulinzi.
Katika habari iliyotolewa Alhamisi polisi wa kimataifa-Interpol wamesema oparesheni hiyo iitwayo Mamba III inawakilisha uchunguzi wa miezi miwili inayowalenga watu wanaoshukiwa kutengeneza, kusambaza na kuuza madawa bandia katika nchi za Burundi, Tanzania, Uganda, Kenya na Rwanda.
Interpol imesema uvamizi huo wa polisi ulifanyika kwa siku mbili katika Afrika ya Mashariki. Shirika hili limesema uchunguzi wao kwa ushirikiano na shirika la afya duniani na kikosi cha kupambana na vitu bandia unaendelea na oparesheni hiyo kupambana na madawa bandia ya kuzuia malaria, chanjo na Antibiotic. Interpoli pia ilisema maafisa walikamata kiasi kikubwa cha madawa ya serikali ambayo yaliingizwa kwa njia za panya.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!