Searching...
Tuesday, August 17, 2010

Babangida kuwania urais wa Nigeria

Uchaguzi wa urais kufanyika mwakani
Uchaguzi wa urais kufanyika mwakani
Aliyekuwa kiongozi wa kijeshi nchini Nigeria, Ibrahim Babangida, ametangaza kuwania urais katika uchaguzi wa mwaka ujao.
Amesema kutokana na uzoefu wake ana uwezo wa kukabiliana na matatizo ambayo yanaikumba nchi hiyo.
Babangida aliitawala nchi hiyo kati ya mwaka 1985 hadi 1993 baada ya kuongoza mapinduzi ya kijeshi.
Baada ya kustaafu alikabidhi uongozi kwa serikali ya muda.
Pamoja na Babangida kiongozi mwingine muislamu kutoka kaskazini mwa nchi hiyo anayepania kuchaguliwa na chama tawala cha People's Democratic Party kwa teketi hii ya urais ni aliyekuwa makamu wa rais, Atiku Abubakar.
Rais wa hivi sasa, Goodluck Jonathan -- aliyechukua hatamu za uongozi baada ya kifo cha rais Umaru Yar'Adua mwezi Mei mwaka huu hajatangaza kuwania kiti hicho hadi sasa.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!