Searching...
Saturday, July 17, 2010

Wakimbizi 2000 warejeshwa Rwanda

Wakimbizi wa Rwanda

Wakimbizi wa Rwanda waliorejea nchini mwao kutoka kambi za Uganda wanasema kuwa walidhulumiwa kwa kurejeshwa kwa lazima. Wanasema kuwa polisi nchini Uganda waliwakamata kwa nguvu na kuwasafirisha kwa malori huku wakiwapiga risasi wale waliojaribu kutoroka.

Watu wawili walijeruhiwa walipojaribu kuruka kutoka malori yao. Zaidi ya wakimbizi 2000 wamerejeshwa nchini Rwanda kutoka Mbarara magharibi mwa Uganda.

Serikali ya Uganda imesema kuwa watu hao hawakuwa wakimbizi halali bali walikuwa wanatafuta hifadhi katika mazingira bora kiuchumi, na kuwa waliagizwa waondoke Uganda kufikia mwanzo wa mwezi huu
Habari na Bbcswahili

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!