Searching...
Thursday, July 22, 2010

Raia mwenye asili ya kisomali ashitakiwa Marekani

Mahakama moja ya Marekani.

Mahakama moja ya Marekani.

Maafisa wa Marekani wamemfungulia mashitaka ya ugaidi kijana mmoja, anayeshtumiwa kujaribu kujiunga na kundi moja la wanamgambo lenye makao yake Somalia na ambalo lina ushirika na al-Qaida.

Mawakala wa serikali ya Marekani mashariki mwa jimbo la Virginia, Jumatano walimkamata kijana huyo mwenye umri wa miaka 20, Zachary Chesser, na kumfungulia mashtaka kwa kusaidia kupeleka vifaa kwa al-Shabab, kundi lenye msimamo mkali wa ki-Islam, ambalo linajaribu kuiangusha serikali dhaifu ya Somalia inayoungwa mkono kimataifa.

Maafisa wa Marekani walisema Chesser, ambaye pia anajulikana kama Abu Talhah Al-Amrikee, alikamatwa Julai 10 wakati akijaribu kupanda ndege kutoka New York kuelekea Uganda, baada ya jina lake kugunduliwa kwenye orodha ya serikali, ya watu waliopigwa marufuku kusafiri.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!