
Waziri wa Afya wa Cameroon Mama Fouda amewataka wananchi katika eneo hilo la kati mwa Afrika wawe waangalifu na kuripoti kesi zozote za kipindupindu mara moja. Nchi za kati mwa Afrika kwa kawaida hukumbwa na magonjwa kama hayo kutokana na umasikini mkubwa ulioko katika nchi za eneo hilo. Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa nchi nyingi za katikati mwa Afrika zinaongoza kwa umasikini barani Afrika zikilinganishwa na nchi za maeneo mengine ya bara hilo.
0 comments:
Post a Comment