Searching...
Friday, July 2, 2010

Ghana kufa na kupona leo

Kevin-Prince Boateng
NYOTA wa kikosi cha timu ya taifa ya Ghana Black Stars leo wanaingia uwanjani kufa na kupona kupigania kuandika historia mpya ya timu za Afrika katika mchezo wa robo fainali wa michuano ya fainali za 19 ya kombe la Dunia zinazoendelea huko ‘Bondeni’ Afrika Kusini dhidi ya washindi wa kombe hilo mwaka 1930, Uruguay.

Mchezo huo unaotarajiwa kuwa wa vuta nikuvute unapigwa majira ya saa 3:30 kwa saa za Afrika Mashariki kwenye uwanja mkubwa wa Soccer City uliopo jijini Johannesburg huku Ghana wakiwa ndiyo wawakilishi pekee wa Afrika waliosalia kwenye michuano hiyo baada ya kusukumwa nje kwa timu zingine tano akiwemo mwenyeji Afrika Kusini.

Asamoah Gyan
Nyota wa timu hiyo Dede Ayew na Jonathan Mensah wataukosa mchezo huu kutokana na kutumikia adhabu ya kadi mbili za njano walizoonyeshwa kwenye michezo iliyopita huku nahodha John Mensah naye akiwa kwenye hatihati ya kuwemo dimbani kutokanana na kuwa majeruhi


Kocha wa timu hiyo tayari ameshatangaza mikakati muhimu ya kuhahakisha anafuzu kwa duru la nusu fainali ya michuano hiyo na kuandika historia mpya hasa baada ya kupata hamasa kubwa ya ushangiliaji kutoka kwa mashabiki wa soka wa Afrika Kusini ambao timu yao imeshatupwa nje ya michuano hiyo.
Habari Bofya hapa

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!