Searching...
Friday, July 23, 2010

Benki za India zawabagua Waislamu kwa kutowapa huduma muhimu

Sample ImageWatetezi wa haki za wafuasi wa dini za wachache nchini India wamekosoa vikali ubaguzi unaofanywa na mabenki ya nchini humo katika kutoa huduma zao kwa wafuasi wa dini ya Kiislamu. Shirika la Kusimamia Haki za Wachache nchini India limethibitisha juu ya kupokea malalamiko mengi ya Waislamu kuhusiana na ubaguzi unaofanywa dhidi yao. Shirika hilo limeeleza kuwa, baadhi ya mabenki yanakataa kutoa huduma mbalimbali zikiwemo za kufungua akaunti na kuwapatia huduma nyingine muhimu Waislamu wa nchi hiyo. Taarifa hiyo inaeleza kuwa, Waislamu wa India wananyimwa kupata suhula za masomo pamoja na nafasi za ajira katika jimbo la Utta Pradesh lililoko kusini mwa nchi hiyo. Waislamu wanahesabiwa kuwa ni kundi la waumini wachache nchini India na wanaonekana kuwa masikini zaidi kuliko wafuasi wa dini nyinginezo. Inafaa kuashiria hapa kuwa, hali inayowakabili Waislamu nchini India ni mbaya zaidi kitabaka kuliko makundi ya Wahindu nchini humo

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!