Searching...
Saturday, July 17, 2010

Afrika Kusini yaomba ujumbe usio wa kudumu wa Baraza la Usalama

Sample ImageSerikali ya Afrika Kusini imeliomba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liichague nchi hiyo kuwa mjumbe asiye wa kudumu wa baraza hilo hapo mwakani. Bi Maite Nkoana- Mashabane Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Afrika Kusini amesema mjini New York makao ya Umoja wa Mataifa kwamba nchi hiyo ikiwa ni urithi wa Nelson Mandela Rais mstaafu wa Afrika Kusini na shujaa wa mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini humo, inapaswa kupewa ujumbe usio wa kudumu wa Baraza la Usalama hapo mwakani. Maite Nkoana- Mashabane amesema kuwa, katika hali ambayo imepangwa kuwa siku ya Jumapili inaadhimishwa kama ni siku ya kimataifa ya Nelson Mandela, nchi zote wanachama wa Umoja wa Mataifa zinapaswa kuchukua mkakati wa kuichagua Afrika Kusini kuwa mjumbe asiye wa kudumu wa Baraza la Usalama. Afrika Kusini iliwahi kuwa mjumbe asiye wa kudumu wa baraza hilo kuanzia mwaka 2007 hadi 2008.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!