Searching...
Saturday, June 5, 2010

Washindi wa Nobel wataka ziwepo sheria bora za kumlinda mwanamke

Profesa Wangari MaathaiWashindi wawili wa tunzo ya amani ya Nobel wamesema kwamba, sheria za kitaifa zinapaswa kurekebishwa ili kuwarahisishia wanawake kuthibitisha kwamba ni wahanga wa jinai za kijinsia hasa katika mahakama kimataifa ya jinai.
Hayo yamesemwa na Profesa Wangari Maathai wa Kenya aliyeongeza kwamba wanawake katika baadhi ya mataifa kama vile Sudan, Kenya na Burma bado wanangojea uadilifu upatikane nchini kwao. Maathai amesema kwamba nchini Kenya mwanamke mmoja tu ndiye alifanyiwa vipimo na kuthibitisha kwamba wanawake walibakwa katika machafuko ya baada ya uchaguzi nchini Kenya mwaka 2008. Hivyo Bi. Maathai amezitaka nchi nyingine kuhakikisha kwamba zinatunza vyema rikodi na nyaraka zinazohusu kesi za ubakaji.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!