Watoto wakionesha uwezo wao wa kuruka sarakasi.
Watoto na wadau mbalimbali leo walihudhuria Siku ya Mtoto wa Afrika iliyofanyika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni “Imarisha familia mtoto apate haki yake”.Mmoja wa watoto waliohudhuria tamasha hilo akionesha umahiri katika wa kuruka ‘samasoti’.
Mwanafunzi wa darasa la tatu shule ya msingi Uhuru Mchanganyiko, Miriam Chirwa, anayetamba na kibao cha Elimu ni Mwanga akikonga nyoyo za wageni waalikwa.
Mtoto Haji Twalib aka DJ Nuni akiimiliki mitambo kuhakikisha burudani ya muziki inatawala.
Sehemu ya wageni waalikwa wakipiga makofi kushangilia burudani ya watoto.
Mmoja wa watoto akipita jukwaani kuonesha ubunifu wa mavazi.
Mtoto Irene akimlisha keki Kamishna Mkuu wa Ustawi wa Jamii, Dunford Makala, kulia ni Miss Universe namba nne mwaka huu, Mwajabu Juma, akipiga makofi.
Habari na Globalpublisher










0 comments:
Post a Comment