Maharamia Wasomali wakiwa na maguruneti ya roketi aina ya RPG wameteka nyara meli ya mizigo yenye bendera ya Panama katika Ghuba ya Aden. Meli hiyo inawahudumu 24 raia wa Bangladesh, Ghana, Misri na Pakistan.Kwa mujibu wa kikosi cha wanamaji cha Umoja wa Ulaya kinachopambana na maharamia Navfor, meli hiyo ijulikanayo kama MV QSM Dubai imetekwa nyara mapema leo Jumatano.
Meli hiyo ilikuwa imetoka Brazil na ilitekwa nyara katika eneo ambalo vikosi vya wanamaji vya Ulaya na Marekani vinalinda doria. Maharamia Wasomali wamekuwa wakiteka nyara meli katika Bahari Hindi na Ghuba ya Aden na kudai vikomboleo vya mamilioni ya dola kabla ya kuziachilia meli na wahudumu wake.


0 comments:
Post a Comment