Leo ni siku ya kimataifa ya bahari, uhifadhi na umuhimu wake,kauli mbiu ya mwaka huu ikiwa "bahari zetu, fursa na changamoto".
Katika kuadhimisha siku hii Katibu Mkuu wa Umoja wa Mtaifa Ban Ki-moon amehimiza serikali na wanachi kote duniani kutambua umuhimu wa bahari kwa binadamu na kuhakikisha kwamba uharibifu wa bahari utokanao na shughuli za binadamu unasitishwa.
Maisha ya bahari yanakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo uvuvi wa kupindukia, mabadiliko ya hali ya hewa na kutupwa kwa taka za sumu mambo ambayo yanatishia mazingira ya bahari.
Ban amesema bahari ina nafasi muhimu katika maisha ya binadamu hasa katika maendeleo endelevu, na wanasayansi kufanya utafiti.


0 comments:
Post a Comment