Searching...
Tuesday, June 22, 2010

Kenya nayo yasajili simu za mkononi kama Tanzania

Matumizi ya simu ya mkononi Kenya

Matumizi ya simu za mkononi yamezidi nchini Kenya

"Namba ya simu ambazo itakuwa hazijasajiliwa mpaka mwishoni mwa July zitakatwa"

Kenya imeanza kazi ya kusajili simu zote za mkononi ikiwa ni miongoni mwa juhudi za kupambana na uhalifu unaotokana na matumizi ya simu hizo.

Watu wanaotaka simu za mkononi watatakiwa kuonyesha hati na anuani za mahali wanapoishi kabla ya kupatiwa namba ya simu. Namba ya simu ambazo itakuwa hazijasajiliwa mpaka mwishoni mwa July zitakatwa, serikali imesema.

Wachambuzi wanasema watu wengi nchini humo wanaunga mkono hatua hiyo ya serikali, kwa matumaini kuwa itasaidia polisi kupambana na uhalifu. Magenge yanayoteka watu nyara katika miji mikubwa mara nyingi yanatumia namba za simu zisizosajiliwa kutuma SMS zinazodai malipo.

Kenya ina watumiaji wa simu za mkononi wapatao millioni 20. Tanzania tayari imeanza zoezi kama hilo la kusajili simu za mkononi.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!