Mjumbe wa kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China ambaye pia ni naibu mwenyekiti wa baraza la mashauriano ya kisiasa la China Bw. Wang Gang na makamu wa rais wa Kenya Bw. Kalonzo Musyoka tarehe 3 wamehudhuria sherehe ya uzinduzi wa chuo cha Confucius cha Chuo Kikuu cha Kenyatta.
Bw. Wang Gang alipotoa hotuba alisema, kuimarisha mafunzo na matumizi ya lugha za nchi tofauti kunasaidia kuhimiza mawasiliano kati ya tamaduni tofauti, na kuimarisha maelewano na urafiki kati ya wananchi wa nchi mbalimbali. Bw. Wang alisema ana matumaini kuwa kutokana na juhudi za China na Kenya, chuo cha Confucius cha Chuo Kikuu cha Kenyatta kitapata mafanikio zaidi, na kutoa mchango katika kuendeleza uhusiano wa kirafiki kati ya China na Kenya, na kuimarisha mawasiliano na ushirikiano kati ya watu wa nchi hizo mbili.


0 comments:
Post a Comment