Searching...
Saturday, June 26, 2010

ATISHIA KUJIRUSHA KUTOKA KWENYE NGUZO YA UMEME!!

Alipoona wanazidi kumsumbua, aliamua kupanda juu zaidi.
Kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Frank Macha, 17, mwanafunzi wa kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari ya Manzese, asubuhi ya leo amefanya tukio lililowashangaza wengi katika eneo la Ubungo Mataa, jijini Dar es Salaam, baada ya kupanda kwenye nguzo kubwa zinazopitisha umeme wa msongo mkubwa, na kutishia kujirusha hadi chini.
Haijafahamika sababu hasa ya kijana huyo kufikia uamuzi huo, lakini alipohojiwa na waandishi wa habari eneo la tukio alidai ni kwa sababu ya ongezeko la mafisadi hapa nchini, ambao serikali imeshindwa kuwachukulia hatua. Kijana huyo ambaye ni yatima, aliokolewa na Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji, na kuteremshwa na ‘winchi’ maalum kutoka kwenye nguzo hiyo.
Frank Macha akiwa juu ya nguzo za umeme huku waokoaji wakijaribu kumshawishi abadili uamuzi wake.
Baadaye, baada ya kazi nzito ya kumshawishi kufanikiwa, alikubali kuingia kwenye winchi tayari kuteremshwa chini.
Frank akiteremshwa chini kwa Winchi maalum kutoka Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji.
Baada ya kuteremshwa chini, alipokelewa na askari polisi waliompeleka kwenye Kituo cha Polisi cha Urafiki kwa mahojiano zaidi.
Umati mkubwa wa watu ulikua ukishuhudia tukio zima lililowasisimua wengi.
Barabara zilifungwa kwa muda kutokana na umati mkubwa wa watu waliofurika eneo hilo kushuhudia kilichokuwa kinaendelea
Habari na Globapublisher

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!