Searching...
Friday, May 28, 2010

Watu wasiopungua 25 wafariki katika ajali ya treni nchini India

Sample ImageWatu wasiopungua 25 wamefariki dunia katika ajali ya treni iliyotokea huko mashariki mwa India baada kutokea mripuko na kusababisha treni hiyo kuacha njia. Ajali hiyo imetokea katika eneo ambalo ni ngome ya waasi wa Kimao ambao ndio wanaoshukiwa kuhusika na mripuko huo. Msemaji wa shirika la reli la India Soumitra Majumdar amesema mripuko huo ulisababisha mabehewa 13 kuacha njia na kuangukia kwenye reli ya treni nyingine ya mizigo. Wakati ajali hiyo inatokea, treni hiyo ilikuwa ikitoka Mumbai na kuelekea Kolkata katika jimbo la Bengal Magharibi. Ajali ya leo ni ya pili kutokea ndani ya wiki hii katika sekta ya usafiri nchini India. Itakumbukwa kuwa watu 158 walifariki dunia siku ya Jumamosi wakati ndege moja ya shirika la ndege la India ilipoanguka wakati wa kutua katika uwanja wa ndege wa Mangalore

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!