Searching...
Saturday, May 29, 2010

Umoja wa Mataifa: Watu 60 wameuawa hivi karibuni nchini Somalia

Sample ImageUmoja wa Mataifa umesema kwamba raia 60 wameuawa na wengine 14,300 kuyakimbia makaazi yao katika mapigano ya hivi karibuni kati ya vikosi vya serikali ya Somalia na wanamgambo wanaoipinga serikali.
Andrej Mahecic msemaji wa Shirila la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Wakimbizi amesema kwamba, kwa mujibu wa taarifa walizopata, watu wasiopungua 60 wameuwa na zaidi ya wengine 50 wamejeruhiwa katika mapigano hayo. Mehecis aidha ameongeza kwamba, makumi ya maelfu ya Wasomali waliokimbia makaazi yao bado wamekwama na kuhangaika katika mji Mkuu Mogadishu huku wanawake na watoto wakilazimika kuomba omba ili kukidhi mahitaji yao.
Idhaa ya kiswahili redio tehran

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!