Searching...
Tuesday, May 25, 2010

Afrika Kusini yaanzisha mahakama ya kesi za kombe la dunia

Sample ImageMsemaji wa Wizara ya Sheria ya Afrika Kusini ametangaza kuwa tayari zaidi ya mahakama 50 zimeundwa katika kila pembe ya nchi hiyo ili kushughulikia kesi zitakazojitokeza wakati wa kinyang'anyiro cha kombe la dunia katika mchezo wa soka kinachotarajiwa kuanza rasmi Juni 10. Tlali Tlali ameongeza kuwa makumi ya korokoro yamejengwa katika miji 10 kunakotarajiwa kuchezwa mechi za michuano hiyo ili kukabiliana na uhalifu wa aina yoyote. Msemaji huyo wa Wizara ya Sheria amesema kuwa kutokana na hali mbaya ya kiusalama inayoshuhudiwa mara kwa mara nchini humo pana haja ya kuimarisha kabisa uwezo wa vyombo vya usalama na sheria katika kipindi hiki. Hii ni mara ya kwanza kwa bara la Afrika kuandaa mashindano ya kombe la dunia katika mchezo wa soka.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!