Searching...
Tuesday, May 25, 2010

Abidjan- Ongezeko la uchumi wa Afrika kwa mwaka 2010 latazamiwa kufikia 4.5%

Shirika la Ushirikiano wa kiuchumi na Maendeleo(OECD) na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AFDB) tarehe 24 zilitoa ripoti ikisema, ingawa mwaka 2009 dunia nzima ilikumbwa na msukosuko wa fedha, ongezeko la uchumi wa bara la Afrika bado linatazamiwa kufikia 4.5% mwaka 2010.

Ripoti hiyo yenye kichwa kisemacho "mustakabali wa uchumi barani Afrika wa mwaka 2010" ilisema, ongezeko la uchumi wa Afrika litadumu hadi mwaka 2011; kufuatia kufufuka kwa uchumi wa dunia, katika mwaka 2011, ongezeko la uchumi barani Afrika litafikia 5.2%.

Ripoti hiyo ilisema, msukosuko wa fedha umevuruga matokeo ya kupambana na umaskini yaliyopatikana katika nchi nyingi za Afrika. Benki ya AFDB inaona kuwa ili kufikia kiwango kilichowekwa na lengo la maendeleo ya milenia ya Umoja wa Mataifa, bara la Afrika linahitaji kuwekezwa dola za kimarekani bilioni 50 kila mwaka.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!