Searching...
Wednesday, April 28, 2010

Semina ya mwisho kwa washiriki wa kili music award 2010


Meneja wa bia ya Kilimanjaro (TBL) George Kavishe akifafanua jambo mbele ya wasanii waliochaguliwa kuwania tuzo za Kili Music Awards 2010 katika nyanja mbalimbali za sanaa,kwenye semina ya mwisho kwa washiriki hao iliofanyika kwenye hotel ya Paradise,jijini Dar jana jioni.
Mkurugenzi wa kampuni ya One Plus Commonication ambayo pia ni moja ya waratibu wa tuzo za Kili Music Awards 2010,Fina Mango akifafanua jambo na pia kumkaribisha muwakilishi kutoka baraza la sanaa la Taifa,kufafanua baadhi ya mambo kwenye semina ya wasanii waliochaguliwa kwenye kinyang'anyiro cha tuzo hizo,ambazo safari hii zimekuwa na muonekano mpya na wenye msisimko mkubwa kwa wanamuziki wenyewe na hata wapenzi/washabiki wa muziki hapa nchini.
Muwakilishi wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Mzee Angelo Luhala akiwaonyesha wasanii nembo ya Baraza la Sanaa la Taifa na pia aliongelea kuhusu baadhi ya wanamuziki ambao waliamua kujitoa kwenye tuzo hizo kwa sababu wanazozijua wao,aidha aliongeza kwa kuwashauri wanamuziki kuwaheshimu mashabiki na wapenzi wao waliowachagua,"hawapaswi kuwaangusha kwa namna moja ama nyingine,kikubwa ni kuonesha na kukubali thamani yao kwako,Wanamuziki tusikubali kujiangusha wenyewe kwa mambo ambayo wakati mwingine yanakuwa hayana maana"" alisema Mzee Luhala.
Mtaalam wa kutengeneza Steji akiwaonyesha wasanii namna itakavyokuwa siku hiyo
Mkurugenzi wa kampuni ya One Plus Communication,Fina Mango na Meneja mkuu wa bia ya Kilimanjaro (TBL) George Kavishe wakiwa katika furaha baada ya kufurahishwa na Mzee Luhala.
Msanii Mrisho Mpoto akitoa hoja.
Prezidaa Nyoshi El Sadaat akiimba moja ya nyimbo zake.
AY akiuliza swali
Deo Mwanambilimbi akiuliza swali la kuhusu usafiri wa bendi iwapo yeye atakuwa ameshinda tuzo hiyo.
Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya One Plus wakiwa katika pozz
Wasanii wakiwa wametulia kwa umakini mkubwa kufuatilia Semina hiyo iliyofanyika jana jioni katika hoteli ya Paradise,iliyopo Benjamin Mkapa Tower,jijini Dar
Wasanii mbambali wanaoshiriki kinyang'anyiro cha tuzo za Kili Music Awardsa wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza kwa semina hiyo.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!