Searching...
Friday, April 30, 2010

Benki ya Stanbic kuzindua mfumo wa Benki wa Shariah


Mkurugenzi Mkuu wa Stanbic Bank, Bashir Awale (kushoto) na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki hiyo Abdallah Singano wakizungumza katika mkutano na waandishi wa habari leo.
Stanbic Tanzania, moja kati ya benki zinazoongoza hapa nchini, inatarajia kuzindua mfumo wa benki unaofuata kanuni za Shariah tarehe 4 Mei, 2010.

Mfumo wa benki wa Shariah unaenda sambamba na kanuni za dini ya Kiislamu, ambao unakataza upokeaji na ulipaji wa riba. Pia uwekezaji wa fedha katika biashara ambazo huendana kinyume na maadili ya dini za Kiislamu hauruhusiwi.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya Stanbic, Bwana Bashir Awale alisisitiza umuhimu wa huduma hii katika nchi hii, hasa ukizingatia uwepo mkubwa wa waumini wa dini ya Kiislamu.

“Tukiwa kama benki inayoheshimu tamaduni na imani za wateja wetu, tumeona umuhimu mkubwa wa kuwa na huduma ya mfumo wa benki wa Shariah nchini. Zaidi ya asilimia hamsini ya watanzania ni waislamu, kwa hiyo ni muhimu kwa benki kuwapatia huduma zinazoendana na matakwa ya imani yao”.

Tanzania itakuwa ni nchi ya kwanza kati ya nchi 17 iliyomo benki ya Stanbic, inayojulikana pia kama Standard Bank, kuanzisha huduma hii.

Uzinduzi huu utashuhudiwa na viongozi na wakurugenzi kutoka makao makuu ya benki ya Standard pamoja na viongozi wa Serikali, wafanyabiashara na viongozi wa dini ya Kiislamu.

“Tunaamini kuwa huduma hii itakuwa na mafanikio makubwa kwa watanzania na kuwa msaada kwa jumuiya ya waumini wa dini ya Kiislamu ambao hawaamini mfumo wa ulipaji na upokeaji wa riba”, alimalizia kusema Bwana Awale.

Kwa taarifa Zaidi:
Abdallah Singano
Head of Marketing and Corporate Affairs
Stanbic Bank Tanzania
+255 754 566944
+255 22 196343
singanoa@stanbic.com

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!