Searching...
Wednesday, September 1, 2010

Kiswahili kimekuwa lugha rasmi ya Kenya

Kwa mujibu wa katiba mpya ya Kenya iliyoanza kutekelezwa tarehe 27, Agosti, Kiswahili sasa kimekuwa lugha rasmi, sawa na Kiingereza. Hii inamaana kuwa Kiswahili kinaweza kutumiwa katika shughuli za kiserikali za Kenya.
Katiba mpya imeagiza kuwa, Kiswahili na kiingereza zote ni lugha rasmi za Kenya, na Kiswahili pia ni lugha ya taifa ya nchi hiyo, hata hivyo ni Kiingereza tu kitakachoendelea kutumika katika shughuli mbalimbali za mahakama kuu na mahakama ya rufaa nchini humo.
Kiswahili, Kiarabu na Kihausa ni lugha kubwa tatu za kiafrika. Kiswahili kinatumika katika nchi za Tanzania, Kenya na Uganda, ambazo ziko sehemu ya Afrika Mashariki. Imechukua muda mrefu kwa Kiswahili kuwa lugha rasmi ya Kenya.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!