Princess Lumy
Kumi na minane ili kuweza kupiga kura
Ni haki ya juu hata weusi waamerika
Leo ni zamu yako dada, kaka kuchagua
Kura yako ndio sauti yako
Mchokozy Ahmedinho
Milolongo vituoni, wameacha zao kazi.
Kura zao mikononi, kuchagua viongozi.
Watujenge maishani, vifaidike vizazi.
mwanati huonekani, kumbe we wakuna nazi?
Princess Lumy
Kamwe huwezi daiwa, mwananchi yako haki
Jiandikishe ka dawa, chukua nafasi kiki
Faida ni yako daima, usitafute bunduki
Ndugu wa Tanzania, mda huo wa mikiki
Mafisadi tumewachoka, nchi yetu kuangamia
Viwango bora kuvifika, kama we wazingatia
Piga kura dada kaka, usije kuugulia
Kilichobaki ni kura yako maana ndio sauti yako
Mchokozy Ahmedinho
Chagua alo na sera, si asali mdomoni.
Mwanadada fanya ghera, utumbukize debeni.
Usihongwe kwa madera, yaso faida mbeleni.
Haki yako piga kura, uwakilishwe bungeni.
Sa usipopiga wewe, mwewe ndo atachukua
Usipatwe na kiwewe, anza mapema chagua
Hii yako dira uwe, maisha bora kupanga
Mi naongea na wewe, piga kura dada kaka
1 comments:
Wonderful!!!!!
Yes, YES WE CAN
Time to vote Tanzania
Post a Comment