Rais Mwai Kibaki wa Kenya amewatumia Waislamu wa Kenya salamu za heri na fanaka kwa munasaba wa kuwadia Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Katika ujumbe wake Rais Kibaki amewatakia Waislamu wote Saum Maqbool na Ramadhan Mubarak. Kibaki ametoa wito kwa Waislamu kuomba dua maalumu kwa ajili ya nchi ya Kenya hasa katika kipindi hiki cha baada ya kumalizika kura ya maoni ambapo nchi hiyo inajitayarisha kutekeleza katiba mpya. Rais Kibaki amesema Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ni kipindi muhimu katika kalenda ya Waislamu kote duniani hasa katika masuala ya kujitolea, kutakasa nafsi na kumtii Mwenyezi Mungu. Rais Kibaki amesema anajiunga na Waislamu wa Kenya kujenga matumaini kuwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani wa mwaka huu utawakumbusha Wakenya wote umuhimu wa kutafakari uhusiano wao na Mwenyezi Mungu na kuwajali wasiojiweza katika jamii.
0 comments:
Post a Comment