Mafuriko yaliyosababishwa na mvua za monsoon nchini Pakistan yanaendelea kukatili maisha ya watu.
Hadi sasa watu zaidi ya 1100 wamefariki dunia na wafanyakazi wa uokozi wanajaribu kuwafikiwa watu 27,000 wanaosemekana kukwama kutokana na mafuriko hayo. Jumla ya watu milioni 1.5 wameathirika na mafuriko hayo, nyumba kusombwa na miundombinu kuharibiwa vibaya.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon jana ameelezea huzuni yake kwa kupotea maisha ya watu wengi kutokana na mfuriko hayo ambayo hajawahi kushuhudiwa Pakistan kwa miaka 80, na ameidhinisha dola milioni 10 kutoka kwenye mfuko wa dharura ili kusaidia katika mahitaji ya waathirika wa mafuriko Pakistan. Msaada huo ni mbali ya ule unaotolewa na mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa. Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limeanza kugawa chakula kwa familia 35,000 kaskazini mashariki mwa Pakistan
0 comments:
Post a Comment