"Nashukuru kwamba Afrika nzima ililaani vitendo vya (magaidi)"
Rais wa Uganda Yoweri Museveni anasema Afrika ni lazima iongeze jitihada zake katika vita dhidi ya ugaidi, kufuatia milipuko ya mabomu iliyouwa watu 76 kampala mwezi huu. Katika hotuba yake Jumapili kwenye ufunguzi wa mkutano wa Umoja wa Afrika, Rais Museveni alitoa wito kwa viongozi wenzake wa Afrika kuwatimua magaidi nje ya bara hilo.
Katika aliyotoa kabla ya mkutano, Rais Museveni alisema majeshi ya Uganda yatawasaka wapiganaji wa kundi la al-Shabab la Somalia, ambalo limedai kuhusika katika mashambulizi ya mabomu ya Julai 11 mjini Kampala.
Katika hotuba yake Rais Museveni alisema "Nashukuru kwamba Afrika nzima ililaani vitendo vya (magaidi)"
Mkutano wa 15 wa viongozi wa Umoja wa Afrika ulianza leo chini ya ulinzi mkali.
Habari na Sauti ya Amerika
0 comments:
Post a Comment