Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imetoa ripoti ikikiri kwa mara ya kwanza kwamba utumwa bado unashuhudiwa nchini humo katika sura ya kisasa.
Duru za habari za Marekani zimeandika kuwa miaka 150 baada ya kufutwa utumwa nchini Marekani Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi hiyo imethibitisha kwamba biashara ya kuuza na kununua wanadamu kama milki nyingine ingali inafanyika nchini humo.
Ripoti ya mwaka huu wa 2010 ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imechunguza kwa ujumla magendo ya wanadamu na hatua za kisheria kuhusu suala hilo nchini Marekani.
Kituo cha habari cha In These Times cha Marekani kimesema kuwa miongoni mwa sababu za kuwepo utumwa wa kisasa ni ukosefu wa usawa katika nchi mbalimbali suala ambalo linazidishwa na masuala ya kiuchumi. Mkurugenzi wa sera wa Muungano wa Kufuta Utumwa na Utoroshaji wa Wanadamu wenye makao yake mjini Los Angeles Stephanie Richard, amethibitisha takwimu za wahamiaji wanaoingizwa Marekani kwa visa sahihi na kusema kuwa wahamiaji hao wanatumiwa kama watumwa.
0 comments:
Post a Comment