Searching...
Friday, July 20, 2012

Man.city, Man.U na Juve zamtaka Van Persie


Van Persie.
Van Persie
Klabu ya Arsenal imepokea maombi kutoka vilabu viwili vikuu vya mji wa Manchester vikitaka kumsajili nahodha wa klabu hiyo Robin van Persie pamoja na klabu ya Italia Juventus.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28 kutoka Uholanzi imearifiwa kuwa hatofuatana na kikosi cha Gunners kinachosafiri kwenda Bara Asia kwa mechi tatu za kujipima nguvu.
Imefahamika kuwa Man.city, United na Juventus zimewasilisha kiango kinachokaribia pauni milioni 15 za Uingereza ingawa Arsenal huenda isikubali ila kiasi kilicho kati ya pauni milioni 25 na 30.
Nahodha na mchezaji bora wa mwaka Van Persie alikataa kuanza majadiliano ya kuongezea mda wake wa kuichezea Arsenal punde baada ya mechi dhidi ya West Bromwich iliyomalizika kwa ushindi wa 3-2 na kuiweka Arsenal kwenye njia ya kushiriki Ligi ya mabingwa barani Ulaya.
Huenda uwezekano wa kushiriki Ligi ya mabingwa ukawa chachu ya Van Persie kukubali kukaa pamoja na shughuli ya usajili wa washambuliaji wawili Lukas Podolski kutoka klabu ya FC Cologne kwa kitita cha pauni za Uingereza milioni £10.9m.
Arsenal ilitarajiwa kumuongezea malipo Mdachi huyo kwa kuandika mkataba wa miaka minne na kumridhisha yeye na familia yake wasiopenda kuhama kutoka London.
Mkataba wa Van Persie unamalizika mwaka 2013 na bado msimamo wake ni ule ule wa kutosaini mkataba mpya.
Mshambuliaji huyo aliyejiunga na Arsenal kutoka klabu ya Feyenoord kwa malipo ya pauni milioni £2.75 miaka minane iliyopita, ameweza kufunga jumla ya mabao 53 katika michezo 53 kwa klabu yake na Taifa katika kipindi cha msimu uliopita

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!